Kubenea akamatwa..aachiwa na kukamatwa tena na polisi Dodoma

JESHI la Polisi mkoani hapa limemkamata tena Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), baada ya kuachiwa huru katika kesi ya kudaiwa kumshambulia Mbunge mwenzake, Juliana Shonza, akiwa bungeni.

Kwa sasa Shonza ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika serikali ya awamu ya tano.

Kubenea anadaiwa kumshambulia Shonza mwaka jana wakati wa Bunge la Julai, wakati mbunge mwenzake huyo akitoka eneo la ukumbi wa Bunge mjini hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alikiri mbele ya waandishi wa habari jana kuwa jeshi hilo limemkamata Kubenea kutokana na kutoridhika na kuachiwa kwake na mahakama.

Alisema wamefanya hivyo ili kumfungulia tena mashtaka mapya juu ya tuhuma hizo.

Muroto alisema kutokana na hatua hiyo Kubenea atafunguliwa kesi mpya inayohusiana na jambo hilo na itaendelea kusikilizwa katika mahakama yamefunguliwa shtaka hilo na sasa litaendelea kusikilizwa tena katika mahakama hiyo kama ilivyokuwa awali.

“Tumemkamata kweli mbunge huyo kwa sababu sheria inaruhusu kufanya hivyo,”alisema Muroto.

Muroto alisema hatua hiyo haina uonevu wowote dhidi ya Kubenea bali sheria zimefuatwa ndio maana amekamatwa kwa mara nyingine kutokana na upande wa pili kutoridhika na uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo.

Alisema kwa sasa shauri hilo litaanzwa kusikilizwa tena kwa mara nyingine katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma.

Mbunge Kubenea alifikishwa mahakamani hapo Julai 4, mwaka jana, akidaiwa kumshambulia Shonza kwenye viwanja vya Bunge mjini hapa.

Baada ya kuachiwa huru jana mahakamani hapo, polisi walimweka chini ya ulinzi Kubenea na kumfungulia kesi nyingine ili ianze kusikilizwa kwa mara nyingine.

The post Kubenea akamatwa..aachiwa na kukamatwa tena na polisi Dodoma appeared first on Mtembezi.


Sponsored by SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini