Simba yamtambulisha Pierre Lechantre kuwa Kocha Mpya

Klabu ya Simba imemtambulisha rasmi kocha wake Mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre pamoja na Kocha wa viungo, Aimen Habibi ambapo leo wamesaini mkataba na klabu hiyo. 

Akizungumza baada ya kusaini mkataba na klabu ya Simba, Lechantre amesema Simba iko vizuri ila inatakiwa kuimarika na kwamba ndiyo sababu ya yeye kufanya kazi na klabu hiyo, huku akiwaahidi wanachama wa Simba ushindi.

Meneja wa Lechantre, Joseph Kamga ametoa wasifu mfupi wa kocha huyo, kwamba aliwahi kuwa kocha bora barani Asia, aliiwezesha timu ya Taifa ya Cameroon kushinda Ubingwa wa Afrika, pia alifundisha timu za Taifa za Qatar, Mali na Kongo.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema Klabu ya Simba inakuwa klabu ya kwanza Tanzania kufundishwa na kocha Mfaransa mwenye uzoefu, ambapo ataanza kazi rasmi ya kukisuka kikosi cha Simba Jumanne ijayo baada ya kurudi kutoka Bukoba.

The post Simba yamtambulisha Pierre Lechantre kuwa Kocha Mpya appeared first on Mtembezi.


Sponsored by SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini