Kamati ya kusimamia mchakato wa sheria mpya ya vyama vya siasa yaundwa

Baraza la Vyama vya Siasa nchini limeunda Kamati ya Sheria na Utawala bora itakayosimamia mchakato wa utungwaji wa sheria mpya ya vyama vya siasa na ubadilishwaji wa kanuni za usajili wa vyama vya siasa, ambayo imepewa muda wa mwezi mmoja kukamilisha ukusanyaji pamoja na kujadili maoni na mapendekezo ya wadau mbalimbali.

Akizungumza baada ya kukamilika kikao cha baraza hilo kilichoshirikisha wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya siasa, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Shibuda amesema  kwa sasa zitaendelea kutumika sheria na kanuni zilizopo hadi pale mchakato wa kutungwa sheria mpya ya vyama vya siasa utakapokamilika.

Shibuda amesema, “Mchakato wa kutungwa sheria mpya ya vyama vya siasa haujakamilika, mchakato wa ubadilishaji wa kanuni za vyama vya siasa haujatekelezwa maoni yanakwenda kuchakatwa baadae yatakuja baraza la vyama vya siasa baada ya kupokea taarifa kutoka kwenye kamati yetu ya baraza kisha tutafanya maboresho kwa minajili ya kutengeneza sheria itakayoleta ustawi wa vyama vya siasa, tunaendelea na kanuni zile zile za usajili wa vyama vya siasa na sheria za vyama vya siasa.”

“Wajumbe wa kikao wameunda kamati ya uongozi na zile zinazohitajika kwa mujibu wa kanuni za kuwepo vyama vya siasa, pia baraza lilikuwa na ajenda saba, ikiwemo kujadili mapendekezo ya kutungwa shera mpya ya vyama vya siasa na kubadili kanuni za usajili vyama vya siasa, kupitia taarifa maalumu ya mwenyekiti wa baraza kuhusu maendeleo ya baraza na ofisi ya msajili wa vyama,” amesema na kuongeza.

“ Pia wamefanya maadhimio ya kujadili mapendekezo ya kutungwa sheria mpya ya vyama vya siasa pamoja na mapendekzo ya ubadilishwaji wa kanuni za usajili wa vyama vya siasa ambapo kamati ya sheria na utawala bora itapokea mapendekezo yaliyokusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali ambao watatoa mawazo ya kutungwa sheria mpya.”

Kamati nyingine zilizoundwa leo na wajumbe wa baraza la vyama vya siasa ni Kamati ya Uongozi wa Vyama vya Siasa ambayo mwenyekiti wake ni Shibuda kutoka Ada Tadea, Kamati ya Fedha itakayoongozwa na John Cheyo kutoka udp, Kamati ya Bunge na Siasa itakayoongozwa na Juju Ndada kutoka NCCR Mageuzi, na Kamati ya Maadili ambayo mwenyekiti wake ni Mohamed Abdalah kutoka Demokrasia Makini.

The post Kamati ya kusimamia mchakato wa sheria mpya ya vyama vya siasa yaundwa appeared first on Mtembezi.


Sponsored by SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini