Walemavu wapatiwa Miguu bandia Dar es Salaam

Zoezi la ugawaji wa miguu ya kisasa ya bandia kwa watu wenye ulemavu wa miguu awamu ya pili limeanza ikiwa ni kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda ya kuwapatia miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji mali kama awali ambapo imejidhihirisha kuwa RC Makonda akiahidi jambo analitimiza kwa vitendo na sio siasa.

Katika awamu ya pili iliyoanza Ijumaa Januari 19, 2018 zaidi ya walemavu 108 wamepatiwa miguu ya kisasa ya bandia ambayo inakadiriwa mguu mmoja unagharimu kiasi cha shilling milioni 2 hadi 3 ambapo yote kwa pamoja ni Sh. milioni 324 lakini kwa jitihada za RC Makonda wamepatiwa miguu hiyo bure.

Katika awamu ya kwanza jumla ya wagonjwa 35 wa kisukari walipatiwa miguu ya kisasa ya bandia yenye thamani ya shilingi milioni 157 kutoka CCBRT na kufanya jumla ya walemavu waliopatiwa miguu hiyo kufikia 143 yenye thamani ya milioni 481 bure.

Baadhi ya walemavu waliopatiwa miguu hiyo wamemshukuru RC Makonda kwa moyo wa pekee wa kuwajali wananchi wake kwa kuzingatia makundi yote kwenye jamii ambapo wamesema kwa sasa wataenda kufanya kazi na kuachana na utegemezi.

Aidha wameishukuru kampuni ya Kamal Group kwa kumuunga mkono RC Makonda kutimiza maono yake ya kuwawezesha walemavu kupata miguu ya kisasa inayowawezesha kufanya shughuli za kujiingizia kipato.

The post Walemavu wapatiwa Miguu bandia Dar es Salaam appeared first on Mtembezi.


Sponsored by SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini