Audio: Abeid Makarabo – Afya ya Roho

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu leo kwa moyo mkunjufu kabisa namtambulisha kwako mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili akitokea jijini Dar es salaam nchini Tanzania ambaye leo anakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo wake uliobeba ushuhuda wa maisha yake uitwao Afya ya Roho, wimbo huu umeandikwa na kuimbwa na yeye mwenyewe huku muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Chosen Records International.

Abeid Makarabo ni kijana wa kitanzania mwenye umri wa miaka 27, ambaye ameamua kuyatoa maisha yake katika kumtumikia Bwana Yesu Kristo kama shukrani ya kumnusuru na mauti baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi yaliyo pelekea kupoteza uwezo wa kutembea (kupooza).

Upande wa kulia ni picha ya Abeid iliyopigwa mwaka 2014 ikimuonyesha akiwa katika hali ya afya na Kushoto ni picha iliyopigwa mwaka 2016 ikimuonyesha akiwa katika hali ya ugonjwa wa kupooza.

Licha ya kuwa katika hali hii ya ugonjwa uliomtesa ka muda mrefu, Abeid hakumuacha Yesu, aliendelea kumtumikia Yesu akiwa kwenye kiti maalumu cha magurudumu (wheelchair ), Ushuhuda wa Abeid juu kile kilichomsibu una mambo mengi ambayo hugusa mioyo ya watu wengi, na ndio sababu ya kuandika na kuimba wimbo huu Afya ya Roho ambao nina hakika hata wewe utakugusa kwa namna yako ya pekee.

Kwa moyo wa wa upendo nakukaribisha sasa kupakua wimbo huu ambao nina imani kubwa kuwa utakubariki na kukuinua katika viwango ambavyo si vya kawaida, Ameen.

Download Link 1 Download Link 2

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Abeid Makarabo kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 763 044 880
Facebook: Abeid Makarabo
Instagram: @abeid_tz
Youtube: Abeid Makarabo

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

share

The post Audio: Abeid Makarabo – Afya ya Roho appeared first on Gospo Media.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini