Video | Audio: Beatrice Kitauli – PANYA

Baada ya kufanya vizuri sana mwaka 2017 kupitia wimbo na video yake iitwayo Wajue akiwa amemshirikisha mwimbaji mkongwe kabisa katika kiwanda cha muziki wa Injili Afrika mashariki na kati Rose Muhando ambayo mpaka sasa inaendelea kufanya vizuri sana kupitia channel yake ya YouTube ikiwa tayari imeshatazamwa mara zaidi ya laki nne, na kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 mwimbaji Beatrice Kitauli ameachia video yake mpya inayobebwa na jina la PANYA, video ikiwa imeongozwa na studio ya Kwetu Studio na muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Eck Production chini ya mikono ya prodyuza Eck Nyongoto.

PANYA ni wimbo uliotumia lugha ya picha unaoelezea kuwa siku zote maadui katika maisha yetu ni watu wanaotuzunguka kila siku na huwa na tabia za panya ambaye anan’gata na kupuliza na ndivyo ilivyo hata katika maisha yetu ya kawaida maadui wanaotuzunguka ni watu ambao wanatutendea mabaya bila hata sisi kujua kwa kuwa huja na kujionyesha na kuishi nasi kama watu wa karibu kimwili lakini kiroho ni maadui wakubwa, hivyo ni vyema kujenga uhusiano mzuri na Yesu ili aweze kukufunua na kuwatambua wale ambao wana mipango mibaya ya juu ya kuharibu maisha yako ili uweze kuwatenga pembeni na kubaki na marafiki walio wema katika maisha yako.

”Enyi rafiki zangu Panya ghalani mwangu mliingia na kupavuruga, mnaong’ata na kupuliza ghalani mwangu mliingia na kupavuruga ni nyie marafiki waongo, wasengenyaji na waua ndoto, mlitafuna mbegu zangu mlifilisi ghala langu Panya… Usikubali kuliwa na Panya maishani mwako, jenga urafiki na Jehova ufike mbinguni… kisha yeye atakuonyesha rafiki wa kweli, anayetafuna mafanikio yako mtenge pembeni” – Haya ni baadhi ya mashairi aliyoyaimba Beatrice Kitauli katika wimbo huu.

Kwa mujibu wa mwimbaji Beatrice Kitauli alisema:-

”Wimbo huu nimeutunga katika ubunifu wa hali ya juu ukiwa katika fumbo la marafiki wabaya wenye tabia kama za panya za kung’ata na kupuliza… ujumbe ulioko kwenye wimbo huu ni kwamba tuombe Mungu atuonyeshe marafiki wazuri wa kuambatana nao katika safari ya mbinguni…. na tujiepushe na marafiki wabaya maana marafiki wabaya huaribu tabia njema…. Panya ametumika kama kifananisho cha tabia ya marafiki wabaya wenye tabia ya kutafuna mafanikio ya wenzao…”

Wimbo huu utakuwa kwenye albamu yake mpya yenye mkusanyiko wa nyimbo tano ikitarajiwa ingia sokoni hivi karibuni.

Nina imani kuwa utabarikiwa na kuinuliwa na ujumbe huu wa pekee ambao kwa hakika umewasilishwa vyema na mtumishi huyu wa Mungu kwa njia ya uimbaji, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Beatrice Kitauli kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 757 830 451
Facebook: Beatrice Kitauli
Instagram: @beatrice_kitauli
Youtube: Beatrice Kitauli

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

share

The post Video | Audio: Beatrice Kitauli – PANYA appeared first on Gospo Media.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini