Ikiwa ni siku tano zimepita tangu Diamond Platnumz ashinde tuzo mbili za Hipipo nchini Uganda, Msanii huyo maarufu zaidi Afrika Mashariki amepokea tuzo nyingine maalumu na ya heshima ‘Plaque’ iitwayo Nyota wa Mchezo ambayo hutolewa na kituo cha redio cha Times FM kupitia kipindi cha The Playlist.
Tuzo hiyo ambayo hutolewa mara moja kwa mwaka kwa wasanii wawili yaani msanii wa kiume na wakike ambaye amefanya vizuri kwa mwaka husika, Diamond amekuwa msanii wa kwanza kukwara tuzo hiyo.
Vigezo vilivyowekwa na kipindi pendwa cha burudani cha Playlist kinachorushwa na kituo hicho, ni jina la msanii kuchaguliwa kwenye kipengele cha Best International Act (Msanii Bora wa Kimataifa), Best Male Act (Msanii Bora wa Kiume), Most Influencial Act (Msanii Mwenye Ushawishi), na Record Breaking Act (Msanii anayevunja Rekodi) kwenye segmenti yao ya Nyota ya mchezo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Diamond Platnumz ametoa shukrani zake kwa kituo hicho na mashabiki kwa ujumla kwa kuona mchango wake kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa mwaka 2017.
Diamond Platnumz amekuwa msanii wa pili kuchukua tuzo hiyo baada ya Vanessa Mdee kukabidhiwa tuzo hiyo mwishoni mwa mwaka jana.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments