Dk. Ndugulile aagiza uchunguzi wa Afya ya uzazi kwa Wanaume

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Mpoki Ulisubisya kwa kushirikiana na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini (NIMR) kufanya utafiti wa afya ya uzazi ya wanaume ili kubaini sababu ya ongezeko la matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.

Dkt. Ndugulile ametoa agizo hilo mapema leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.

Amesema tafiti za afya zilizofanywa duniani zinaonyesha kuna hali ya upungufu wa nguvu za kiume, unaowakabili baadhi ya wanaume katika mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania.

“Tafiti duniani zinaonyesha kuna hali ya upungufu wa nguvu za kiume, Tanzania haijawahi fanya utafiti kuhusu suala hilo ila ni miongoni mwa nchi zinazoathiriwa na tatizo hilo, inabidi kuangalia afya ya wanaume kwa kufanya utafiti kwa kushirikiana na NIMR ili tujue tatizo ni nini,” amesema.

Aidha, Dkt. Ndugulile ametaja baadhi ya sababu zinazochangia matatizo ya upungufu wa kiume, ikiwemo ulaji wa vyakula vya mafuta, matumizi ya vileo kupita kiwango hususani pombe kali pamoja na kutokufanya mazoezi kwa muda mrefu.

Amesema ili kuepukana na tatizo hilo, wanaume wanatakiwa kufuata lishe bora na kufanya mazoezi kila mara.

The post Dk. Ndugulile aagiza uchunguzi wa Afya ya uzazi kwa Wanaume appeared first on Mtembezi.


Sponsored by SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini