Jaji Mkuu afuta baadhi ya Ada za Kimahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amefuta rasmi ada kwa nyaraka mbalimbali za kimahakama.

Taarifa iliyotolea mchana wa leo na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katarina Revocati kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa Jaji Mkuu amefuta ada kwa nakala za hukumu, uamuzi mdogo, amri, amri itokanayo na uamuzi wa mahakama pamoja na tozo za hukumu za mahakama zitolewazo kwa wadaawa.

“Maelekezo haya yanafuta ada kwa nyaraka zilizotajwa katika ngazi ya mahakama Kuu, mahakama za hakimu mkazi, mahakama za Wilaya na za mwanzo,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Pia, inaeleza kuwa, Prof. Juma amewaelekeza Manaibu Wasajili na Mahakimu Wakazi Wafawidhi kuhakikisha kwamba wanatekeleza maelekezo hayo mara moja kwa kuweka mfumo wa kufuatilia utoaji wa nyaraka hizo kwa wadaawa kwa wakati bila ya malipo yoyote.

The post Jaji Mkuu afuta baadhi ya Ada za Kimahakama appeared first on Mtembezi.


Sponsored by SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini