MAN CITY YAENDELEA KUIMARIKA, MENDY AREJEA KIKOSINI

Mabingwa watarajiwa wa ligi kuu Soka ya England msimu huu klabu ya Manchester City itaendelea kuimarika baada ya wachezaji waliokuwa majeruhi kurejea.


Gabriel Jesus ambaye alikua majeruhi alirejea dimbani Jumamosi wakati Manchester City ilipoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chelsea na sasa City imempokea mazoezini beki wake Benjamin Mendy ambaye alikua na majeraha ya goti Kwa muda mrefu.
Mendy mwenye miaka 23 anayecheza nafasi ya beki wa kushoto alikua katika Mazoezi ya Jana Jumatatu Ikiwa ni Mara ya kwanza tangu alipoumia mwezi Septemba wakati Man City ikicheza na Crystal Palace.
Mendy amerejea muda muafaka wakati Manchester City ikibakiza ushindi wa mechi nne kuweza kunyakua ubingwa wa ligi kuu Soka nchini England msimu huu sambamba na michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini