YANGA YAKUBALI KIPIGO NYUMBANI

Timu ya Yanga imekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka Township Rollers katika mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga itahitaji kushinda mabao 2-0 au zaidi ili kufuzu hatua inayofuata kitu ambacho kinaonekana ni kigumu kwa mabingwa kutokana na mchezo walioonyesha leo.

Townships walipata bao la mapema dakika ya 10 kupitia kwa Lemponye Tshireletsi kabla ya Obrey Chirwa kusawazisha Yanga dakika ya 29.

Dakika ya 83 Motsholetsi Sikele aliifungia Township bao la pili baada ya walinzi wa Yanga kuzembea kuondoa hatari langoni mwao.

Mchezo wa marudiano utafanyika jijini Gaborone wiki mbili zijazo.

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini