MAN UNITED YATUPWA NJE LIGI YA MABINGWA ULAYA

Man Utd 1-2 Sevilla: Mourinho's side crash out of Champions League
Usiku wa jana ulijawa na maumivu makubwa kwa mashabiki wa Manchester United Duniani baada ya timu yao kutupwa nje ya mashindano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya wakifungwa nyumbani bao 2-1 dhidi ya Sevilla kutoka Spain.

United iliingia katika mchezo wa jana na mfumo ambao Wapenda Soka wengi duniani bado wanaona si sahihi kwa timu hiyo iliyokua na lengo la kupata ushindi zaidi huku ikiwaacha benchi Antony Martial, Juan Mata, Scot McTominay na Paul Pogba wakianza Maroane Fellain,Jesse Lingard na Marcus Rashford.

Sevilla walipata mabao yao yote kupitia kwa Wissan Ben Yedder ambaye aliingia kuchukua nafasi ya 72 na kufunga mabao hayo mawili dakika ya 74 na 78 kisha Romelu Lukaku kuipatia United bao la kufutia machozi dakika ya 84.

Kwa matokeo hayo Manchester United United wanaaga mashindano hayo kwa matokeo ya jumla ya bao 2-1 Sambamba na Shaktar Donetski ambao nao jana walifungwa ugenini bao 1-0 na Wenyeji AS roma hivyo kutupwa nje kwa matokeo ya jumla ya bao 2-2 huku Roma wakinufaika na bao la ugenini walilopata katika mechi ya awali 



Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini