TSHISHIMBI WA YANGA NDIYE BORA ZAIDI KWA MWEZI FEBRUARI

Kiungo wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayeichezea yanga ya Dar es salaam Papy Kabamba Tshishimbi ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania baada ya kiwango bora alichokionyesha akiwa na timu yake.

Mchezaji huyo anayemudu vyema nafasi ya kiungo ametwaa tuzo hiyo akiwashinda Emanuel Okwi wa Simba na Pius Buswita pia wa Yanga akiwa amefunga mabao matatu na kuisaidia yanga kuzoa Pointi 12 katika mwezi huo.

Ametangazwa jana na amejishindia zawadi ya kiasi cha milioni moja pamoja na decoda ya king'amuzi cha AZAM TV 
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini