MESSI AFIKISHA MABAO 100 BARCELONA IKIIADHIBU CHELSEA MABINGWA ULAYA

Barcelona 3-0 Chelsea: Messi masterclass dumps Blues out of Europe
Mategemeo ya timu za England kuweza kuingia kwa wingi katika hatua ya Robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya yametoweka baada ya jana tena Chelsea kutupwa nje ya michuano hiyo dhidi ya Barcelona kwa kufungwa bao 3-0.

Lionel Messi ndiye aliyeleta tofauti jana usiku akifunga mabao mawili huku akitengeneza bao moja kuweza kuitupa nje Chelsea kwa ushindi wa jumla wa bao 4-1 baada ya mechi ya awali kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Messi jana alifikisha mabao 100 katika historia ya michuano hiyo ikiwa ni mabao 17 nyuma ya Cristiano Ronaldo anayeongoza kwa ufungaji katika historia ya michuano hiyo mikubwa zaidi katika ngazi ya klabu 

Tayari timu 8 zimejulikana ambazo zimetinga katika hatua ya Robo fainali baada ya Bayern munich nao kushinda ugenini jana kwa bao 3-1 dhidi ya Besiktas timu hizo ni Juventus,Manchester City,Liverpool,Bayern Munich, Real Madrid, Sevilla, AS Roma na Barcelona na ratiba itapangwa kesho Ijumaa.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini