POGBA HATIHATI KUIKOSA SEVILLA

 
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho hana uhakika kama kiungo wake Paul Pogba atakuwa fiti katika mchezo wa maruadiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya Sevilla.

Mreno huyo amesema kuelekea mchezo wa kesho utakaofanyika katika uwanja wa Old Trafford hana uhakika wa kupata huduma ya Pogba.

"Nitaongea nae kujua anaendeleaje, aligongana na mwenzake mazoezini siku ya Ijumaa na hakuweza kumaliza mazoezi.
"Atafanyiwa uchunguzi ili kuweza kufahamu ukubwa wa tatizo ambapo kwa sasa siwezi kusema kama atacheza au la," alisema Mourinho.

Mourinho ameutaja mchezo dhidi ya Sevilla kama muhimu kuliko ule dhidi ya Liverpool kwakua utakuwa wa kufa na kupona ili kutinga robo fainali ya michuano hiyo.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini