SKY WAMPIGA UMEME CARRAGHER KWA KUMTEMEA MATE SHABIKI.

Legend' wa Liverpool Jamie Carragher amesimamishwa kazi na kituo cha talevisheni cha Sky Sports anachokifanyia kazi kama mchambuzi baada picha za video kumwonesha akimtemea mate shabiki wa Manchester United.

Nyota huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza alilazimika kuomba radhi baada ya picha kusambaa  ikimwonesha akitemea katika gari ambalo alikuwemo binti mwenye umri wa miaka 14 baada ya ushindi wa jana wa Man United dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Old Traford

Carragher amekua akichambua soka katika kituo hicho tangu mwaka 2013 alipotundika daluga kama mchezaji lakini sasa itabidi aondoke kidogo mbele ya kamera za Sky Sports kuanzia usiku wa leo ambapo alitarajiwa kuweo katika show ya Monday Night Football.

Taarifa ya Sky imesema wamekichukulia kitendo hicho kwa uzito mkubwa na wanataka Jamie aelewe kwamba amefanya jambo la hali ya chini kulinganisha na heshima ya kituo chao.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini