TOTENHAM YABORONGA NYUMBANI YATUPWA NJE MABINGWA ULAYA

Tottenham 1-2 Juventus (3-4 agg): Paulo Dybala scores winner
Kipigo cha bao 2-1 walichokipata Tottenham hotspur dhidi ya mabingwa wa italia Juventus kimewaondoa katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya Msimu huu na sasa watatakiwa kusubiri mpaka msimu ujao kujaribu tena bahati yao.

Ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Wembley Spurs ilikubali kufungwa bao hizo 2-1 katika mechi ya pili ya hatua ya 16 bora hivyo kuondoshwa kwa jumla ya bao 4-3 baada ya mechi ya awali jiini Turin kumalizika kwa sare ya bao 2-2.

Son Hueng-min alitangulia kuipatia Tottenham Bao la kuongoza dakika ya 26 tu ya mchezo bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko na dakika ya 63 Gonzalo Higuain aliendelea kuitesa Spurs baada ya kufunga bao la kusawazisha kisha Paulo Dyabala kuongeza la pili dakika tatu badae.

Juventus sasa inaungana na Liverpool,Manchester City na Real Madrid katika hatua ya Robo fainali huku zikisubiriwa mechi za mwisho za timu zilizobaki ambazo zitachezwa wiki ijayo.



Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini