Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo Janja ambaye ni mume halali wa muigizaji wa filamu bongo Irene Uwoya, amesema wimbo wake wa 'Wayuwayu' ni dongo maalumu kwa watu waliokuwa wanaiponda ndoa yake bila ya kujua undani wao ulivyo.
Dogo Janja amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuwepo maneno mengi yaliyokuwa yanamponda msanii huyo na mke wake ambapo watu wengi walikuwa wanaisema vibaya ndoa ya wawili hao kuwa hawaendani kwa kila kitu.
"Walitokea watu walikuwa wanakejeli na kuongea mambo kibao, na kuonekana mimi kidagaa sina chapaa wananitukana lakini mwisho wa siku nawakanyaga kama soksi zangu 'so' wimbo wa Wayuwayu ulikuwa ni sehemu ya kufikisha maudhui kwa watu waendelee kuheshimu mahusiano ya watu na wala wasiangalie tofauti zao zilizopo", amesema Dogo Janja.
Pamoja na hayo, Dogo Janja ameendelea kwa kusema "kwenye mahusiano kitu pekee kinachozingatiwa ni upendo, kama watu mnapendana na kuheshimiana vitu vingine ni vya kawaida, binadamu wamekuwa wamekuwa na tabia ya kuhukumu vitu kwa nje lakini hawaujui undani vizuri kwa hiyo ilikuwa moja ya kufikisha ujumbe na burudani pia kwa mashabiki zangu"
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments