Wafanyabiashara Ufaransa kuja ‘kumulika’ fursa

UJUMBE wa wafanyabiashara 40 kutoka Ufaransa unatarajiwa kuwasili mwezi ujao kwa ajili ya kuona fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini.

Hayo yamebainishwa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier alipotembelea ofisi za kampuni ya magazeti ya Serekali (TSN) ambayo huchapisha magazeti ya ‘Habari Leo’, ‘Daily News’ na ‘SpotiLeo’.

Balozi Clavier amesifu juhudi zinazofanywa na magazeti hayo kwa jili ya kuelimisha wananchi pamoja na juhudi ya kueleza fursa mbalimbali zilizopo nchini kupitia Jukwaa la Biashara linaloandaliwa na TSN ambalo litafanyika Zanzibar Machi 15, mwaka huu. Kutokana na uhusiano uliopo baina ya nchi hizi mbili, mwanadiplomasia huyo amewakaribisha Wafanyabiashara wa Tanzania kwenda kuwekeza nchini Ufaransa.

Pia, Balozi Clavier ameahidi kuboresha mahusiano baina ya waandishi wa habari wa TSN na waandishi wa habari wa Ufaransa kubadilishana ujuzi na uzoefu ikiwa ni jitihada za kuendeleza mahusinao ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa TSN, Dk Jim Yonazi amemshukuru balozi kwa kutembelea ofisi hizo na kuahidi ushirikiano zaidi na vyombo vya habari vya Ufaransa katika kubadilishana uzoefu na ujuzi. Katika mkutano huo, Balozi Clavier alikuwa ameambatana na ofisa habari wa ubalozi wa Ufaransa, Iku Kasege. Mbali na Dk Yonazi, TSN pia imewakilishwa na Naibu Mhariri Mtendaji Tuma Abdallah na maofisa wengine wa kampuni hiyo.

The post Wafanyabiashara Ufaransa kuja ‘kumulika’ fursa appeared first on Mtembezi.


Sponsored by SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini