Wakulima Mkoani Kagera : Bora Tulime Baangi Kuliko Kuuza Kahawa

Wakulima Mkoani Kagera : Bora Tulime Baangi Kuliko Kuuza Kahawa
Wananchi na wakulima wa kahawa mkoani Kagera wamelalamikia suala la kukamatwa wakati pindi wanapokuwa sokoni wakiuza zao hilo na kusema kuwa kuliko kuuza kahawa bora walime bangi kwani wakulima wa zao hilo hawako huru kwa sasa.



Wakulima hao wamefunguka hayo wakati wakizungumza na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof. Anna Tibaijuka ambapo wamesema kuwa zao la kahawa halina uhuru kwani wafanyabishara hao wanahusishwa na biashara za magendo kwa kile walichodai kuwa hakuna magendo yanayofanyika kwa watu wa ndani.

“Tunaomba hili zao letu lipewe uhuru, ndani ya nchin hakuna biashara ya magendo huwa ni kubadilishana tu ninakupa mahindi unanipa kahawa, nakupa kahawa unanipa ndizi”, amesema mmoja wa wananchi.

Akizungumza na wananchi Prof. Tibaijuka, amesema kuwa amekuwa akizungumzia sana suala la kahawa bungeni, kwakuwa bila kahawa hakuna maendeleo mkoani humo.

“Mimi kama mbunge wa Muleba Kusini, nitawatetea wakulima na sikubaliani na kuzuia watu kuuza binafsi, kilio changu juu ya zao la Kahawa hata Rais Magufuli anafahamu”, amesema Prof. Tibaijuka

Hayo yanajiri baada ya  Serikali mkoani humo kutangaza kuwa  kahawa yote itakusanywa kupitia kwenye Vyama vya Ushirika na kupelekwa sokoni Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo wanunuzi wote watanunulia hapo mnadani, kwa mantiki hiyo hakuna mkulima yeyote atakayeruhusiwa kuuza kahawa nje ya mfumo wa ushirika.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini