Msanii wa filamu, Salma Jabu aka Nisha Bebee amefunguka kwa kudai kwamba hawezi kudate na mwanaume ambaye hana pesa kwa madai hawana shukrani.
Muigizaji huyo ambaye pia ni mfanyabiashara, amedai wanaume wengi waliopita kwake walikuwa wanampenda kwaajili ya pesa lakini sio mapenzi ya kweli.
“Nimeshadate tayari na watu ambao hawana mtonyo lakini mwisho wa siku hawana shukrani,” Nisha aliimbia Bongo5. “So kwa sasa hivi siwezi kudate na mtu ambaye nimempita kipato, lazima awe amenipita,”
Aliongeza, “Wanaume wengi ambao walikuwa wanakuja kwangu walikuwa wanataka mpaka kununuliwa nguo, kila wiki wanataka shopping ya nguo, baby sijui nimeona kitu fulani kizuri, sijui nataka kile halafu mwisho wa siku hawana mapenzi wa kweli,”
Muigizaji huyo amesema kwa sasa amempata mwanaume wa kizungu ambaye amedai anaona anaweza kufika naye mbali zaidi kimaisha.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments