Msanii wa muziki wa Bongo fleva na hitmaker wa ngoma ya ‘Muziki’ Sharifa Thabeet maarufu kama Darassa amekanusha taarifa za kupotea kisa matumizi ya madawa ya kulevya.
Baada ya kuhit sana na ngoma yake Darassa alikuja kupotea ghafla na mara moja kuna tetesi zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Darassa amejiingiza Kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na kwa muda mrefu alikuwepo Rehab.
Global Publishers wanaripoti kuwa baada ya uchunguzi wa muda mrefu maripota wao walifika katika eneo analoishi ambapo lilikutana moja kwa moja na Darassa mwenyewe akiwa amembebelea mtoto wake wa kike huku hali yake kiafya ikiwa safi tofauti na inavyoenezwa.
Huyu ndiye mwanangu, maneno yamesemwa sana lakini huyu ndiye aliyenifanya kukaa chini kwa muda na kulea,” alisema Darassa huku akimbembeleza mwanaye huyo mwenye miezi kadhaa.
Lakini pia GPL wanaripoti kuwa baada ya Kuchonga na kukanusha Tetesi za madawa ya kulevya Darassa aliwatembeza maripota katika mjengo wake wa kifahari:
Hii hapa ni studio yangu, maisha yangu yote yapo hapa, huwezi kunikuta nikitamba studio yoyote, vitu vyote napikia hapa”.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments