Hamisa Mobetto “Watakao Nitukana Sitawashughulikia Mimi Ila Sasa hivi Kuna kitengo maalumu "

Hamisa Mobetto “Watakao Nitukana Sitawashughulikia Mimi Ila Sasa hivi Kuna kitengo maalumu "
Siku ya leo August 30, 2018 Mwanamitindo Hamisa Mobetto, msanii Barnaba, mchekeshaji Dullavani pamoja na muimbaji Shilole wamekula shavu la kuteuliwa na Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA CCC) kuwa mabalozi wa kampeni ya ‘Be Smart’ inayojihusisha na kuelimisha vijana kuondokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii mashuleni.

Wakati wa utambulisho wa wasanii hao kila mmoja alipata nafasi ya kuongea na kuulizwa maswali na waandishi wa habari ndipo ilipofika zamu ya Hamisa Mobetto ambaye alijibu swali la muandishi kuhusu kutukanwa kwake mtandaoni je atachukua hatua yeyote ya kisheria au atasamehe..?

Hamissa Alijibu Hivi "Kila binadamu ameumbwa na moyo tofauti ila moyo wangu huwa ni mgumu huwa nasamehe naendelea na maisha yangu ila kwa sasa nikitukanwa kitengo maalum kinapambana nao kwakua hata TCRA hawapendi matusi na hata watakaonitukana sasa hawatakuwa mikononi mwangu"
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini