WAKALI kunako muziki nchini Nigeria, Tekno, Mr. Flavour na mchekeshaji Gordon wamenusurika kifo baada ya ndege waliyokuwa wamepanda kupata hitilafu wakiwa angani.
Mchekeshaji Gordon ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoa taarifa hizo kupitia ukurasa wake kwenye Mtandao wa Instagram ambapo alisema ishu nzima ilitokea Agosti 25, mwaka huu wakiwa njiani kutoka Lagos kuelekea Accra kwa ajili ya shoo. “Samahani, nisaidieni kuniombea na kumshukuru Mungu. Mungu amejibu kwangu, Mr. Flavour, Tekno na vijana wa bendi tuliokuwa tumeongozana nao kutoka Lagos kuelekea Accra.
”Mungu ametuokoa na ajali. Dakika nane tukiwa angani, rubani alitutangazia kuwa ndege yetu imepata hitilafu kubwa, tunamshukuru Mungu tumenusurika kifo,” aliandika.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments