JESHI la Polisi Mkoa wa Tabora limewakata watu watatu kwa matukio tofauti akiwemo dereva aliyekuwa akiendesha Treni ya abiria huku akiwa amelewa na wengine wawili walikutwa wakisafirisha madawa ya kulevya aina ya Bhangi.
Taarifa ya Polisi iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo imemtaja Dereva aliyekamatwa akiendesha treni ya abiria akiwa amelewa kuwa ni Elirehema Macha mkazi wa Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Emanuel Nley alisema kuwa dereva huyo alikamatwa wiki iliyopita baada ya kuendesha treni ya abiria namba B 12 iliyokuwa ikitoka Dar es salaam kuelekea Kigoma akiwa amelewa na kutosimama kusimama katika kituo cha Malongwe.
Aliongeza kuwa kitendo cha dereva kutosimamisha treni kwenye kituo hicho kulileta taharuki kwa abiria waliokuwa wakitelemka na wale waliokuwa wakitaka kupanda ndipo taarifa ikatolewa polisi ambao waliweza kumkamata.
Katika tukio jingine Kamanda Nley alisema Polisi imekamata na madawa ya kulevya Amos Maziku ambaye ni Ajenti wa mabasi na Hassan Selemani dereva ambao walikutwa kwenye Kituo cha mabasi Sagara cha mjini Nzega wakiwa na Bhangi kilogram 51.45 wakiisafirisha.
Kamanda Nley alisema kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha bhangi hiyo kwenye basi la Shabco lenye namba za usahili T 501 BRZ lililokuwa likielekea jijini Mwanza huku wameweka ndani ya Ndoo kubwa ya maji na wamefunga ndani ya mifuko ya Sandarusi wakiwa wamechanganya na sufuria na sahani ili wasijulikane.
Aidha Kamanda huyo alisema katika misako inayoendelea wamefanikiwa kukamata Silaha mbili zilizotengeneza kienyeji
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments