Nuh Mziwanda: Siwezi Kumpongeza Shilole Kwa Kujenga Nyumba


Msanii wa muziki wa bongo fleva, Nuh Mziwanda amefunguka na kudai hawezi kumpongeza aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Shilole, kwa kuweza kujenga nyumba ya kuishi licha ya kwamba alikuwa anafahamu juu ya jambo hilo.


Nuh ametoa kauli hiyo jana alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa nakituo cha  EATV, na kusema kwamba anayepaswa kutoa pongezi au kumtia moyo wa faraja ni mumewe Uchebe nasio yeye.


"Siwezi kuzungumzia chochote kuhusiana na suala la Shilole kujenga nyumba. Mimi sitaki kuongea mambo ya Shishi halafu siwezi kumpa moyo kuhusu nyumba moyo atapewa na Uchebe sio mimi japo nilikuwa najua kuwa Shishi anajenga", amesema Nuh.


Kauli hizo za Nuh zimekuja ikiwa zimepita takribani siku nne tokea mwanadada Shilole, kuweka picha mtandaoni ikiwa inamuonyesha yupo katika harakati za kumaliza ujenzi  wa nyumba hiyo.


Mbali na hilo, Nuh Mziwanda amefafanua kuwa sio kweli nyimbo yake aliyoitoa hivi karibuni amemshirikisha Ben Pol, bali kazi hiyo wamefanya wote pamoja kwa maana ni kazi yao wote.

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini