Elimu ya Chuo Kikuu ni moja ya malengo ya wanafunzi wengi shuleni ambayo pia huhesabiwa kama moja ya kilele muhimu cha safari ya kielimu. Nchini Tanzania elimu imeganyika katika mtindo wa elimu ya awali, ya msingi, ya sekondari na ya chuo. Katika ngazi ya chuo nako kumegawanyika kwani vipi vyuo ambavyo hutoa vyeti na diploma na vipo vile ambavyo hutoa shahada (digrii). Hapa chini tumekuwekea orodha ya vyuo vikuu bora nchini Tanzania vinavyotoa shahada. Orodha hii imezingatia pamoja na mambo mengine idadi ya tafiti ambazo chuo hufanya kwa mwaka, uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi, machapisho (publications), heshima katika majukwaa ya elimu ya kimataifa pamoja na mambo mengine. Orodha hii ni kama ifuatavyo.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Hiki kiko jijini Dar Es Salaam na ndicho chuo kikongwe zaidi nchini. Kilianzishwa mwaka 1970.
2. Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)
Chuo hiki kiko mkoani Morogoro na kilianzishwa mwaka 1984. Kinatoa elimu hasa katika mambo ya tafiti za kilimo, chakula, mifugo na teknolojia katika mambo hayo.
3. Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU)
Kama ilivyo kwa SUA, hiki nacho kinapatikana mkoani Morogoro. Awali kilifahamika kama IDM-Mzumbe lakini kikapanda ngazi na kuwa chuo kikuu mwaka 2001. Kina matawi katika maeneo mbalimbali nchini.
4. Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
Chuo hiki kinapatikana Jijini Dodoma na kilianzishwa mwaka 2007. Kama ilivyo kwa UDSM, SUA na MU, vyuo hivi vyote vinamilikiwa na serikali.
5. Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
Chuo hiki nacho ni mali ya serikali, kinapatikana jijini Dar Es Salaam na kilianzishwa mwaka 1963.
6. Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU)
Chuo hiki kinapatikana jijini Dar Es Salaam. Kinamilikiwa na serikali na kilianzishwa mwaka 2007.
7. Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST)
Chuo hiki kilianzishwa mwaka 2010, kiko jijini Arusha. Kinamilikiwa na serikali.
8. Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU)
Hiki kilianzishwa mwaka 1997, zamani kikiitwa Mikocheni International University. Umiliki wake ni binafsi na kinatoa hasa elimu ya tiba katika kuanzia stashahada hadi shahada ya uzamili.
9. Chuo Kikuu cha Tumaini (TU)
Hiki kinamilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kilianzishwa mwaka 2007. Kinapatikana mtaa wa Ikungi Jijini Dar Es Salaam. Kina matawi katika maeneo mbalimbali nchini.
10. Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT)
Chuo hiki kinamilikiwa na Kanisa Katoliki Tanzania. Kinapatikana mkoani Mwanza lakini pia kina matawi katika maeneo mbalimbali nchini. Kilianzishwa mwaka 2002.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments