Serikali ya Afrika Kusini Ijumaa imeomba msamaha kwa wakulima wa kizungu kwa ‘mawasiliano mabaya’ kuhusu uwezekano wa kuchukuliwa ardhi zao ili kuharakisha mageuzi ya kilimo na kuweka sehemu kubwa ya mashamba kwenye mikono ya watu weusi.
Kuomba huko msamaha huo kumekuja mwanzoni mwa mchakato wa utaratibu wa mashauriano juu ya mageuzi ya ardhi utakaofanyika nchi nzima .
Miaka 24 baada ya kumalizika kwa zama za ubaguzi, sehemu kubwa ya mashamba ya biashara nchini humo bado yanamilikiwa na wazungu, ambao ni asilimia 8 tu ya raia wa nchi hiyo.
Kauli ya Mkurugenzi
Mkurugenzi mtendaji wa Kilimo, Mike Mlengana amesema kuwa pendekezo la marekebisho ya katiba ili kuruhusu ardhi kuchukuliwa bila ya kulipia fedha lilitafsiriwa vibaya na ‘mshambulizi’ kwa wakulima wa kizungu.
Mkusanyiko wa wakulima wazungu na weusi katika jimbo la Limpopo umezungumzia masuala mengi kuhusu miradi ya mageuzi ya ardhi ambayo yanasukumwa na wakulima wazungu. Baadhi yao tayari wametoa ardhi zao kwa watu weusi na wanawasaidia kuwapatia maelekezo ili kuweza kuwa wazalishaji kamili wa chakula kwa ajili ya biashara.
Serikali ya ANC
Mlengana anasema ni bahati mbaya kwamba serikali ya African National Congress (ANC) mpaka sasa imepuuza juhudi nyingi zinazofanywa na wakulima wa kizungu.
Amebaini kuwa waziri wa kilimo, Senzeni Zokwana amewabeza maafisa wa serikali kwa kushindwa kuwatoa khofu wakulima wa kizungu kwamba ardhi zao zitachukuliwa.
“Waziri anasimama na kusema nyinyi maafisa wa serikali, kwanini hamjakwenda huko na kuzungumza na wakulima? Hakuna kitu kama hicho! Hili mmelipata wapi kuwa sisi tunakuja na bunduki na kuchukua mashamba ya wakulima wa kizungu,” amesema Mlengana.
Mlengana pia anasema orodha inayosambaa kuwataja wakulima wazungu 139 wanaomiliki mashamba kuwa yatachukuliwa na serikali, “imepotoshwa.”
Wamiliki wa ardhi 139
Anasema wamiliki ardhi 139 wameiomba serikali kuwalipa fedha nyingi kwa ardhi zao, kwa hiyo serikali itaiomba mahakama kuliangalia suala hilo ili bei muafaka itolewe kwa mashamba hayo.
Mlengana amesisitiza kwamba wakulima wazungu wana maisha nchini Afrika Kusini.
Mkurugenzi mtendaji anasema hali ya baadaye ya kilimo nchini Afrika Kusini ni wakulima wazungu na weusi kufanya kazi pamoja, na kufadhiliwa na serikali na kuongezea kuwa mpaka hivi sasa wamekuwa wakitumia fedha zao wenyewe kwa mageuzi ya ardhi; wakati huu mmekuwa mkijaribu kufanikisha mageuzi ya kweli ya ardhi, kuna fedha za serikali ambazo najaribu kuzielekeza kwenye ushirika.
Shutuma za rushwa
Katikati ya shutuma za kusambaa kwa rushwa ndani ya utaratibu wa mageuzi ya ardhi. Mlengana amesema idara yake ya kilimo ina nia ya dhati kufanya kazi kwa ufanisi na kushughulikia vyema fedha za walipa kodi zitumike vizuri.
Wakulima wazungu katika mkusanyiko wamelalamika huku wakiahidi kurekebisha makosa yaliyo kuwepo wakati wa enzi ya ubaguzi. Kama mmoja alivyofafanua, “baba zetu wameiba ardhi, na kama tukipewa fursa, tutairejesha. Lakini kwa wakulima weusi wenye ujuzi ambao wana nia ya dhati ya kuzalisha chakula kwa ajili ya nchi.”
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments