Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Khalid Mohamed aka TID amefunguka kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya na changamoto katika muziki wake.
Siku za nyuma TID ameshawahi kushika headlines kwa kutumia madawa ya kulevya na hata kukiri kuwa alikuwa muhanga wa madawa.
Kwenye mahojiano na Bongo 5, TID amefunguka na kusema kipindi anatumia madawa ya kulevya alipoteza vitu vingi sana na anatamani kukabidhiwa rungu la kuwarekebisha wanaotumia madawa ya kulevya na alimtolea mfano Chid Benz.
Mimi nikabidhiwe Chid Benz nikae naye maana amekuwa akitusumbua kwa muda sasa kwa sababu wanampeleka rehab akitoka anarudia yale yale lazima kutakuwa kuna kitu wanakosea kama kweli wananmjali wafanye kitu tofauti kama hawamjali wamuache tu kama wanavyomuachaga.
Chid Benz is true talent and was a successful guy halafu tumekorofishana tu alivyoingia kwenye vitu hivyo halafu mimi namuona kama bado ana nafasi kama binadamu hakuna mtu ambaye anafeli akafurahi”.
Siku za nyuma TID ameshawahi kushauri Chid Benz akanatwe na achapwe ndio atasikia na kuacha madawa kwani watu kadhaa wameshajatibu kumpeleka rehab lakini amekuwa akirudia madawa wakati wote.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments