Malkia wa filamu, Jacqueline Wolper Massawe amenunua kopi moja ya albamu ya ‘Gold’ ya Muimbaji Barnaba Classic kwa dola 3000 sawa na tsh milioni 7.
Hayo yamefanyika kwenye listening party ya albamu hiyo uliofanya Alhamisi hii katika ukumbi mmoja ulio karibu na hotel ya Sea Cliff Masaki jijini Dar es salaam.
“Kabla ya mimi kuwa bosi lady alikuwa anakuja kesho events zangu na kufanya show bure, kwahiyo Barnaba kwangu ni mtu muhimu sana, nimenunua hiyo albamu kwa dola 3000 kama kumsupport kwa sababu kwangu ni mtu muhimu,” alisema Wolper.
Katika shughuli hiyo ambayo iliwakutanisha wadau mbalimbali wa muziki, ulikuwa na burudani za kutosha ambapo pia MC Pilipili ndio MC wa shughuli hiyo ambayo ilianza saa 7 jioni hadi saa 16 usiku.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments