Trump Ametishia Kuiondoa Marekani

Trump Ametishia Kuiondoa Marekani
Rais Donald Trump ametishia kuitoa Marekani katika Shirika la biashara Duniani WTO iwapo shirika hilo litashindwa kubadilisha utendaji wake kwa nchi hiyo.

Rais Trump amekuwa akishinikiza sera zinazoitetea nchi yake akisema kuwa Marekani inashuighulikiwa isivyo sawa na shirika hilo.

Shirika hilo la Biashara duniani lilianzishwa kwa ajili ya kusimamia sheria za biashara duniani na kutatua tofauti kati ya nchi. Onyo lake hilo la kutaka kujitoa katika Umoja huo umeonesha mvutano uliokuwepo kati ya sera za kibiashara za Rais huyo na mfumo wa biashara huru ambao shirika hilo unasimamia.

Kama hiyo haitoshi hivi karibuni Marekani ilipinga uchaguzi wa majaji wapya wa mfumo wa WTO wa kukabiliana na mashauri jambo ambalo linaweza kudhorotesha uwezo wa kutoa hukumu.

Mwakilishi wa Marekani katika masuala ya biashara Robert Lighthizer naye amekuwa akiinyoshea kidole WTO kwa kuingilia mamlaka ya Marekani.

Katika siku za hivi karibuni Trump alinukuliwa pia akisema kuwa endapo ataondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye basi uchumi wa Marekani utaporomoka na kila mwananchi atakuwa maskini.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini