Mshambuliaji wa timu ya Mwadui FC, Salimu Aiyee ambaye alimfunga Klaus Kindoki, amesema kuwa anajutia kwa nini walipoteza mchezo huo nyumbani licha ya kutengeneza nafasi nyingi.
Aiyee alimalizia mpira uliomponyoka Kindoki baada ya Salum Ilanfya kuachia shuti kali lililomshinda Kindoki kwa kulitema ndipo Aiyee akamalizia kwa guu lake la kulia.
"Jambo jema kuifunga Yanga, ila sijafurahishwa na timu yangu kupoteza tukiwa nyumbani licha ya kutengeneza nafasi nyingi hivyo tutahakikisha tunakuwa makini katika michezo yetu mingine inayofuata ili tushinde," alisema.
Kindoki alitolewa na kocha mkuu Mwinyi Zahera kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Ramadhani Kabwili, akiwa benchi alionekana akitokwa machozi.
Mwadui wamepoteza michezo 4 na kutoa sare 3 na wamepoteza michezo 7 kati ya 14 waliyocheza mpaka sasa, wakiwa na pointi 13.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments