Klabu ya soka ya Simba kupitia kwa nahodha wake, John Bocco, imeeleza kuwa matokeo ya suluhu na Lipuli FC hayakuwa matokeo waliyoyatarajia bali walijitahidi kutengeneza nafasi lakini hawakuzitumia vizuri.
"Haikuwa matarajio yetu kwa matokeo tuliyoyapata, tulijitahidi kutengeneza mashambulizi lakini haikuwa bahati yetu. Tunaangalia kipi tulichokosea, tunaenda kujirekebisha ili tufanye vizuri kwa mchezo unaokuja"- John Bocco.
Jana baada ya mchezo huo, kocha wa Simba Patrick Aussems alisema wachezaji wake walikuwa wanawaza sana mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Mbambane Swallows utakaopigwa Jumatano ijayo kitu ambacho kiliwapotezea umakini dhidi ya Lipuli FC.
''Kipindi cha kwanza hatukucheza sana, wachezaji wangu walikuwa wakifikiria kuhusu mchezo wa klabu bingwa siku ya Jumatano, kipindi cha pili tulipata nafasi nyingi lakini tukazipoteza'', alisema Aussems.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments