Yanga Wataka Kindoki Aongezewe Muda

Yanga Wataka Kindoki Aongezewe Muda
Licha kuonesha kiwango duni ambacho hakikuwafurahishwa wengi katika mechi ya ligi dhidi ya Mwadui FC, mashabiki na wanachama baadhi wa Yanga wameuomba uongozi wa klabu hiyo kumpa muda Klaus Kindoki.

Kindoki alicheza mechi hiyo akichukua nafasi ya Beno Kakolanya ambaye aligoma kusaifiri kuelekea Shinyanga kwa madai ya mshahara, alifungwa bao la kusawazishwa wakati Yanga ikiwa imetangulia, bao ambalo wengi waliamini ni la kizembe.

Mashabiki hao baadhi wametoa yao ya moyoni na kueleza kuwa hiyo ni sehemu ya mchezo pekee na inahitaji kipa huyo kupewa muda zaidi ili kuzoea ligi ya Tanzania namna ilivyo.

Katika mechi hiyo, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo mabao yake yaliwekwa kimiani na Heritier Makambo pamoja na Mrisho Khalfan Ngassa.

Kwa sasa Yanga tayari imeshawasili mjini Kagera tayari kwa maandalizi dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo ambao utapigwa Uwanja wa Kaitaba kesho Jumapili.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini