Kwa muda sasa tangu tamasha la tigo fiesta limeanza na mpaka sasa linakaribia kumalizika , kumekuwa na pengo kubwa sana kwa tamasha hilo na kila kitu kinachoendelea ambacho kilizoewa kufanywa kwa utaratibu mzuri pengine hasa katika ufahamu mzuri zaidi kutokana na ukweli kuwa Bosi Ruge Mutahaba alikuwa ana mchango mkubwa sana katika tamasha hilo.
Ruge alikuwa akizunguka na wasanii katika kila mikoa kuhakikisha kuwa wasanii wamekuwa katika wakati mzuri wa kufurahia tamasha lakini pia kuhakikisha mashabiki pia , lakini pia alikuwa mtu wa kujitoa sana katika jamii ukiachilia mbali mawazo yake yaliyokuwa yenye thamani kila semina ya kila mkoa aliyokuwa akienda.
Kama utakumbuka kuwa tangu mwezi june bosi huyu amekuwahaonekani katika media na kazini pia kama wanavyosema wafanyakazi wake, swala ambalo liliwaumiza wengi kutokana na kwamba ugonjwa uliomshika alihitaji muda mrefu wa mapumziko kuliko kazi.
Gadner g Habash anaelezea swala la kutokuwepo kwa Ruge jinsi lilivyoweka pengo kubwa sana katika msimu huu wa fiesta kwa sababu ukweli uatabaki uwa alikuwa mtu mwenye mchango mkubwa sana kwa tamsha, kwa wasanii na hata mashabiki zake pa.
Sponsored by
ZAMOTO MEDIA
0 Comments