Yanga yaibuka na ushindi, Kindoki alia uwanjani


Yanga imeibuka na matokeo ya mazuri katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara nje ya uwanja wa taifa msimu huu na kujisongeza juu zaidi katika msimamo wa ligi.


Mchezo huo uliopigwa katika dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga, umeshuhudia Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC.

Mabao ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji Heritier Makambo dakika ya 10 na Mrisho Ngassa katika dakika ya 55 huku bao pekee la Mwadui Fc likifungwa na Salim Aiyee katika dakika ya 40 ya mchezo.

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera aliwatoa Gadiel Michael na Klaus Kindoki baada ya kipindi cha pili kuanza na nafasi zao kuchukuliwa na Mateo Anthony golikipa Ramadhan Kabwili.

Lakini katika hali ya kushangaza, Klaus Kindoki alitokwa na machozi wakati akitoka nje ya uwanja, jambo lililowashangaza watu wengi.

Baada ya mchezo huo, sasa Yanga inashika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kwa jumla ya alama 29 katika michezo yake 11 iliyocheza huku nafasi ya kwanza ikiongozwa na Azam FC. Mpinzani wake wa karibu, Simba imeshuka hadi nafsi ya tatu kwa alama 26.

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini