Harmonize awa gumzo njiani akielekea Mtwara kwa ajili ya Wasafi Festival

Harmonize awa gumzo njiani akielekea Mtwara kwa ajili ya Wasafi Festival
Msaniii wa muziki wa kizazi kipya kutoka katika lebo ya muziki ya WCB, Harmonize amekuwa gumzo akiwa njiani kuelekea Mtwara ambako ndio linafanyika tamasha la Wasafi Festival litakalofanyika Jumamosi hii. Msanii huyo amekutana na mashabiki wake njiani wakati anaelekea Mtwara kwani yeye aliwahi kuondoka jana na wasanii wenzake wa Wasafi wakiondoka leo alfajiri.



Kupitia katika moja ya post zake msanii huyo amesema kuwa anatangulia kwa ajili ya kuibua vipaji ambavyo bado havijafanikiwa kutoka kisanaa.

Haya ndio maneno yake ” HIZI NI AMSHA AMSHA ZA NJIANI TUU USIOGOPE SIJAFIKA HATA MTWARA
BADO NDIOKWANZA NIMELALA
MASASI ILI KUHAKIKISHA NAPATA WALE WASANI WENZANGU AMBAO
HAWAJAPATA NAFASI YA KUSIKIKA
BADO KUPITIA #wasafifestival2018
WATAPATA NAFASI YA KUONYESHA UWEZO WAO PALE NANGWANDA TAREHE 24 USICHOKIJUA NI KWAMBA NJIA YOTE YANI TOKA DAR MPAKA NIMEFIKA #MASASI
WOTE WANAJUA KINACHOENDELEA MTWARA NI NINI….!!!! NA WAPO TAYALI…!! NINA WASI WASI NA ULE UWANJA KUTOTOSHA 🤗 …!!!! HAYA WANANGU WA MASASI TUKUTANE STEND KUU KUANZIA SAA (6) MCHANA HUU NAHITAJI AKINA HARMONIZE (2) WAKAIWAKILISHE #MASASI PALE NANGWANDA KESHOKUTWA TAREHE 24/11/2018 MTWARA …!!”
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini