“Wema uko wapi? Umepatwa na nini?” – Ex wa Wema Sepetu

HABARI ZA MASTAA “Wema uko wapi? Umepatwa na nini?” – Ex wa Wema Sepetu
Mwanamitindo Luis Munana wa Namibia ambae aliwahi kuwa mapenzini na Mwigizaji Wema Sepetu amemkumbuka Wema na kutaka kujua ni kitu gani kimemuweka kimya.

Luis Munana ambaye aliwahi kushiriki shindano la Big Brother Afrika 2014 akiwa na Idris Sultan, amemtaka Martin Kadinda ambaye ni mtu wa karibu na Wema Sepetu kumuelezea kinachoendelea mpaka Wema Sepetu akawa kimya kiasi hicho.

Luis Munana ameandika “Unapokuwa na mahusiano na mtu basi siku zote mtaendelea kuwa na mawasiliano hata kama mkiachana.Hata kama hatuko pamoja ila ninakujali na ni matumaini yangu uko salama maana siku zote huwa nakuwazia mema na kutaka ufurahi“

“Ukimya wako unanipa tabu. Ninachotaka kujua ni kwamba uko salama.@wemasepetu Uko wapi? Kwa nini haujibu msg zangu Whatsapp & DMs? @martinkadindaofficial kuna nini kinaendelea?”
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini