Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Weusi Nikki wa Pili amefunguka mwanzo mwisho kuhusiana na yale aliyoyazungumzo mkongwe na rapa Afande Sele.
Nikki amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagrama na kusema:- “Afande anasema, Weusi tulipata tuzo za kili kwa sababu sisi ni Wachaga……..Tuzo za kili kwa usiku mmoja zilikuwa na zaidi ya kategori 30….ukisema labda kwa miaka mitatu ni tuzo 90….hapo karibuni 99% ya washindi sio wachaga……hivyo ukisema uchaga ni kigezo inamaanisha huna ufahamu dhidi ya tuzo au una ufahamu mdogo……any way nikawaida ya binadamu kuwa na ufahamu mdogo……..kuhusu redio Weusi….tumepigwa na kushika chati ya redio zote tanzania na hata za nje kama Mtv, trace, citizen nakadhalika……ukisema tunabebwa na redio moja pia…..inamaanisha huna ufahamu mzuri juu ya weusi….so ni tatizo lile lile la ufahamu mdogo…………hapa sijakujibu isije tafsirika vibaya…..bali nimefanya uchambuzi wa mpangilio wa mawazo yako…..uchambuzi unanionesha yamepangwa katika ufahamu mdogo…”
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments