Pluijm Awachenjia Niyonzima na Tshishimbi

Pluijm Awachenjia Niyonzima na Tshishimbi
KOCHA Mkuu wa Azam FC , Hans Pluijm hana mpango wa kuwasajili viungo, Haruna Niyonzima wa Simba na Papy Kabamba Tshishimbi wa Yanga kama inavyozushwa.



Viungo hao kwa pamoja wamekuwa wakihusishwa na Pluijm katika usajili wa dirisha dogo baada ya kumsajili Obrey Chirwa ili kuweza kuongeza nguvu katika kikosi hicho.



Niyonzima ambaye alisajiliwa Simba msimu uliopita awali alitokea Yanga ambapo kocha Hans amekuwa akimwelewa vizuri kutokana na uwezo aliokuwa akiuonyesha katika timu yake hiyo ya zamani lakini tangu atue Simba amekuwa akikosa nafasi ya kucheza kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimuandama.



Akizungumza na Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili, Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd amesema; “Nimezungumza na kocha Hans ameeleza kuwa kwa upande wake hawahitaji kina Niyonzima na Tshishimbi katika kikosi chake hivyo atatafuta wachezaji wengine.”



Vile vile amesema kuwa, mchezaji wao Daniel Amoah ameanza mazoezi mepesi baada ya upasuaji aliofanyiwa msimu uliopita na kumfanya akae nje miezi tisa hivyo ataanza kuonekana uwanjani mwezi wa 12 huku wachezaji Frank Domayo na Paul Peter wakiwa wanaendelea na matibabu ambapo watakaa nje miezi miwili.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini