Timu ya Simba yakiri Kuteswa na Lipuli


 Klabu ya soka ya Simba kupitia kwa msemaji wake
Haji Manara, imekiri kuwa bado wanakumbukumbu nzuri na namna ambavyo Lipuli ilivyokuwa klabu pekee iliyogoma kufungwa na Simba katika mechi zote mbili msimu uliopita.
Akiongea kuelekea mchezo wao wa ligi kuu kesho utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam, Manara ameweka wazi kuwa kocha wao Patrick Aussems anatambua uwezo wa Lipuli FC hivyo ameandaa kikosi kwaajili ya kusaka alama 3 na si vinginevyo.

''Tunawajua Lipuli vizuri na tunafahamu ndio timu pekee iliyopata sare pacha msimu uliokwisha wa ligi lakini Simba ndio bingwa wa taifa hili na tunaingia kesho tukiwa kamili hivyo mashabiki wa Simba waje Taifa kesho saa kumi waone mpira wa raha kutoka kwa kocha wetu Aussems'', amesema.

Kwa upande wa Lipuli Fc kupitia kwa msemaji wao Festo Sanga wamesema wamejiandaa vyema kwaajili ya kushindana kutafuta alama 3 dhidi ya wenyeji wao Simba.

Msimu uliopita Lipuli haikufungwa na Simba baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza uwanja wa taifa kabla ya kutoka sare ya aina hiyo kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini