Waziri Tizeba Akabidhi Ofisi Aacha Ujumbe Mzito

Waziri Tizeba Akabidhi Ofisi Aacha Ujumbe Mzito
Aliyewahi kuwa Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba ambaye ni Mbunge wa Buchosa Mkoani Mwanza leo tarehe 22 Novemba 2018 amemkabidhi rasmi ofisi Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa mikutano maarufu kama Kilimo IV Jijini Dodoma na kuhudhuri


Akizungumza katika hafla hiyo Dkt Tizeba amempongeza Hasunga kwa kuteuliwa nafasi hiyo ambapo amesisitiza kuwa wizara inapaswa kuendelea kusomesha wataalamu mbalimbali nchini wakiwemo wa ugunduzi na utafiti ili kuongeza tija ya kilimo na utoaji elimu kwa wakulima na kuongeza uwezo wa uzalishaji wa wananchi sambamba na Taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa Wizara ya kilimo ni tanuru muhimu kwa mahitaji ya wananchi hivyo inapaswa kutazamwa kwa karibu zaidi na serikali ikiwa ni pamoja na kupewa fedha kwa wakati ili kukamilisha miradi mbalimbali ambayo tayari imeanzishwa.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amempongeza waziri huyo mstaafu Mhe Dkt Charles Tizeba ambaye ni Mbunge wa Buchosa kwa kazi kubwa aliyoifanya kwenye wizara ya kilimo ikiwa ni pamoja na kusimamia kwa weledi ukuaji wa sekta ya kilimo .

“Kutokana na alama alizoziacha Dkt Tizeba kwenye wizara ya kilimo hakika tunastahili kumuona kama Mtakatifu kwani kulikuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa chakula nchini lakini alisimamia kidete na kuhakikisha kuwa swala hilo linamalizika na sasa nchi ina ziada kubwa ya chakula hakuna njaa” Amesema Hasunga

Novemba 10 2018 Rais Magufuli alisema "nilimwambia Waziri Mkuu awakumbushe mawaziri wake, kwa sababu matatizo mengi yaliyokuwa yakihusu kilimo na viwanda yalikua yanamalizwa na Waziri Mkuu, nilijiuliza pia kahawa ni kilimo pia vipi Waziri hakuliona pia."

"Nilijiuliza kwanini hawa tuliowapa majukumu hawafanyi hivi, ni ukweli pia bei ya soko la korosho limeshuka kidogo unapoona kuna tatizo unamtuma Waziri Mkuu anatatua," aliongeza Rais Magufuli


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini