Uongozi wa Chama Cha Wanchi CUF unaoungwa mkono na Upande wa Katibu Mkuu wa Chama hicho umeendelea na harakati za kuhakikisha Mahakama inawapatia dhamana makada wake akiwemmo Mbunge wa Kilwa Kusini, Suleiman Bungara pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Habari, Mbarara Maharagande.
Viongozi hao wa CUF walitiwa mbaroni mapema jumanne wiki hii na jeshi la polisi wilayani Kilwa kwa tuhuma za uchochezi, wakiwa kwenye Jimbo la Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Bungra 'Bwege'.
Kupitia mtandao wake wa kijamii, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jussa amesema mapema leo hii viongozi wa Chama hicho wanaendelea na jitihada za kuhakikisha viongozi wao wanapatiwa dhamana.
“Asubuhi hii viongozi wa Chama cha CUF wakiambatana na wadhamini pamoja na wakili watafika mahakama ya Lindi kukamilisha taratibu za dhamana ambazo ziko wazi toka jana kwa ajili ya kuwadhamini Suleiman Bungara (Bwege), Mbarala Maharagande na Abuu Mussa Mjaka.”
Oktoba 2, 2018 akizungumza na www.eatv.tv, Mbunge Bwege alisema yeye huwa haogopi kukamatwa na vyombo vya dola kwa kile alichokidai ameshakamatwa mara kwa mara kabla ya kuwa mbunge.
“Taratibu zote mimi nilifuata na kila kitu nilipeleka polisi, mimi ni mbunge nina haki ya kufanya mikutano, lakini leo asubuhi wameniachia kwa dhamana, kesho tunafanya tena mkutano palepale nilipokamatwa jana mimi sihofii kukamatwa na kama nikiogopa basi niache tu ubunge, kukamatwa sijaanza leo nimekamatwa karibia mara 30 kabla sijawa mbunge”, alisema Bwege.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments