Ikiwa imebaki siku moja tu, kufikia kilele cha tamasha la Tigo Fiesta hapo kesho Novemba 24, 2018 kunako viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam, wasanii wote watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo wameandaa mchezo wa Basketball dhidi wafanyakazi wa Clouds Media Group.
Taarifa iliyotolewa na rapper Wakazi inaeleza kuwa mechi hiyo itafanyika katika viwanja vya Gymkhana kuanzia saa 11:00 jioni.
Fiesta Fever starts today!!! Tunaanza na Allstar Game ya Basketball ya ARTISTS VS CLOUDS MEDIA. Ni Katika viwanja vya Gymkhana (Spiders – Bball Kitaa) kuanzia Saa Kumi Na Moja Jioni (5pm). Wote mnakaribishwa….. kutakuwa na Few surprises as well. Wasanii na Fans njooni mshangilie Kikosi chetu tafadhali, Ushindi ni Lazima.
Catch me on PowerBreakfast & Clouds360 asubuhi hii nikitoa more details about the Game and other exciting this za Grand Finale ya #TigoFiesta2018#MojaKubwaa
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments