Kuwa na Mademu Wazuri Kwangu ni Kawaida :-Msami

Kuwa na Mademu Wazuri Kwangu ni Kawaida :-Msami
Msanii wa bongo fleva nchini ,Msami amefunguka na kusema kuwa kwake kuwa na mademu wazuri ni kitu cha kawaida ingawa watu wamekuwa wakisema kuwa tangu ameachana na Uwoya amekuwa hana umaarufu tena.

Mwanamuziki huyo ambae kwa sasa hasemwi sana kama ilivyokuwa hapo awali , anasemwa kupata umaarufu, kiki na jina sana pale alipokuwa na mwanadada kutoka bongo movies Irene Uwoya.

Hata hivyo yeye mwenyewe anakanusha swala hilo na kusema kuwa katika maisha yake kuwa na wasichana wazuri ni kitu cha kawaida ila tu sio kila kitu mpaka utoe taarifa kuwa kinafanyika.

Wakati mwingine sio lazima kila kitu ukiweke katika mitandao, mimi nina bahati ya kuwa na watoto wazuri tu kikitoka kitu kinaingia kitu kuwa na mademu wazuri kwangu ni kawaida”
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini