Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amefunguka na kuongelea tetesi zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefilisika.
Tetesi hizo zimezidi kupamba Moto sasa hivi kwa sababu Barakah ameonekana kukonda kupita maelezo hali iliyopelekea wengi kufikiria huenda ni kwa sababu ya maisha magumu.
Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha XXL ya Clouds Fm, Barakah amesema kuwa yeye hajawahi kuwa tajiri na hivyo kwasasa ndio ameanza kuitafuta hela yake kwa kuanza kufanya kazi zake mwenyewe huku akidai kuwa yeye sio msanii wa kuweka maisha yake hadharani.
Mimi ni mmoja ya wale artist sipendelei sana kuweka hadharani hali ya uchumi wangu au maisha yangu na ndio maana ni vigumu mtu kujua kama niko sawa Kiuchumi au nimeshuka Kiuchumi kwasababu nina Personal life so naamini pia pesa inatautwa nikiitafuta inakuja na inaweza yakatokea matatizo ikatumika labda vibaya”.
Na sio kama tatizo kubwa sana kwasababu hata makampuni makubwa huwa yanayumba, matajiri wapo wengi kuliko hata mimi na mimi sijawahi kuwa tajiri labda nimefilisiki sijawahi kuwa na hela mimi sasa hivi ndio nataka labda niitafute hela sasa now ndio naenda kuitengeneza hela yangu, kwanza niko nafanya kazi zangu mwenyewe kwasababu mi sio yule artisht wa kuonyesha maisha yangu”.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments