Body spray za Mwana FA ‘FYN by Falsafa’ zimemfikia Rais mstaafu Jakaya Kikwete hii ni baada ya kuziachia rasmi siku chache zilizopita ikiwa lengo lake kubwa ni kuleta manukato kwa jinsia zote mbili.
Mwana FA ametoa ujumbe kupitia ukurasa wake wa instagram na kusema kuwa spray hizo ambazo ni kwaajili ya wanawake pamoja na wanaume (Blue ya kiume na Pink ya kike) zitapatikana madukani wiki ijayo kwa shilingi elfu 4 tu za Kitanzania.
“Uwezekano po… kila wakati…ndoto zinaweza tu kutimia kukizikazania. nawashukuru kwa support na naamini tutafanya vizuri na hii. asanteni sana.”
“Waungwana, ndugu zangu wapendwa, body sprays zetu hizi hapa @FYNbyFalsafa; BLUE ya kiume na PINK ya kike… imagine bei ya jumla ni TZS 4,000 kwa moja, SHANGAA WEWE, na niamini zitafanya unukie vizuri SANA…😀”
“Kuanzia wiki ijayo mzigo utakuwa madukani. Yeyote anayetaka kufanya pre-order ama kuwa msambazaji wasiliana nasi kwa namba +255766170270 au email management@mwanafa.com; nawashukuru kabisa. 🙏🏽”
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments