Waziri Mwakyembe amepokea majina 8 ya wanaokwamisha uchaguzi Yanga

Waziri Mwakyembe amepokea majina 8 ya wanaokwamisha uchaguzi Yanga
Leo Jumatano ya December 19 2018 Mkurugenzi wa michezo wa wizara ya michezo Yusuph Singo ameongea na waandishi wa habari na kueleza kuhusiana na maendeleo ya mchakato wa chaguzi mkuu ndani ya club ya Yanga wakiwemo wanaopanga kukwamisha mchakato huo kwa maslahi yao binafsi.

“Kiukweli tumeafikiana kuwa tulikuwa tunakwenda kufanya uchaguzi kwa kadri tulivyokuwa tumeafikiana, waziri Dar Harrison Mwakyembe amepokea majina ya watu nane yanahusishwa kuhusika zaidi kwenye vurugu au kuhamasisha uchaguzi wa Yanga usifanyike, vikao vinafanyika vya siri sehemu mbalimbali tumezibaini kulingana na maelezo ya Waziri”>>> Yusuph Singo

“Malengo makubwa ya vikao hivyo ni kuhamasisha au kuwafanya wanachama washindwe kufikia lengo au dhamira Kuu kufanya uchaguzi na kupata viongozi wao ambao wataongoza club hiyo, waziri mara tu baada ya kuyapata majina hayo leo asubuhi amechukua hatua yeye mwenyewe ya kuyawakilisha majina hayo kwenye vyombo vya usalama ili uchunguzi ufanyike na endapo watabainika kuhusika kweli hatua stahili zitachukuliwa”>>>Yusuph Singo

Kama utakuwa unakumbuka vizuri mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF Mlangwa Ally ni kuwa uchaguzi mkuu wa Yanga utafanyika mwezi January 13 2019, hiyo ni baada ya zoezi la kuchukua fomu kufungwa rasmi na zoezi la kampeni kwa wagombea kumalizika.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini