Msanii kutoka katika bendi ya Twanga pepeta Charles Baba amefanya sherehe Jumamosi hii na mpenzi wake ambaye alifahamika kwa jina la Mariam na ni baada ya kudumu naye kwa takribani miaka kumi katika uchumba wao.
Amezungumza hayo ndani ya eNewz huku akisisitiza kwamba hayuko tayari kuongea suala lolote kuhusu ndoa zake zilizopita kwa sasa kipaumbele chake ni mke wake Mariam na kusema kwamba anampenda sana na hawezi kumuacha kamwe.
"Nampenda sana mume wangu ni chaguo langu na nimempenda mwenyewe siwezi kubadilisha mawazo yangu na napenda watu wafahamu kwamba nimekuwa katika mapenzi na mme wangu tangu mwaka 2005 mpaka sasa hivyo namfahamu vizuri na mimi ni shabiki wa kazi zake" aliongea mke wa Charles Baba.
Charles Baba amemalizia kwa kusema kwamba pamoja na kwamba imezoeleka kwa wasanii wakioa wanapotea katika muziki lakini kwa upande wake hawezi kuacha muziki kwa kuwa ndio kazi yake lakini pia mke wake amekuwa akimsapoti kwa kiasi kikubwa katika kazi yake hiyo.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments