Marekani Yamzuia Mama Raia wa Yemen Kumuona Mtoto wake Aliye Karibu Kufa

Marekani yamzuia mama raia wa Yemen kumuona mtoto wake aliye karibu kufa
Mama wa mtoto aliye raia wa Yemeni amezuiwa kumuona kijana wake aliye karibu kuaga dunia kutokana na sheria ya kuwazuia wageni kutoka nchini mwake, familia imeeleza.

Mtoto Abdullah Hassan alizaliwa na maradhi ya ubongo ambapo madaktari walisema hataweza kuishi.

Ndugu wanasema mama yake anataka kumuona kwa mara ya mwisho kabla ya kuondoa mashine ya kumsaidia kupumua.

Baba yake anasema mama wa Abdullah hawezi kwenda nchini Marekani kutokana na marufuku iliyowekwa na utawala wa Trump.

Wafanyabiashara wa mtandaoni kulipa kodi Tanzania
Wanamgambo 66 wa al-Shabab wauawa na mashambulizi ya anga
Abdullah na Baba yake ni raia wa Marekani, familia imeeleza.

''Anachotamani ni kushika mkono wa mtoto wake kwa mara ya mwisho'', Baba wa mtoto Ali Hassan aliliambia gazeti la San Francisco Chronicle.

Amesema mtoto atapoteza maisha kama atapelewa Misri, ambako mama yake anaishi kwa sasa.

Mke wa Hassan, Shaima Swileh, anatafuta ruhusa kutoka wizara ya mambo ya ndani ya Marekani ili aweze kuingia nchini humo haraka
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini